RIPORT YA UMOJA WA MATAIFA JUU YA NCHI AMBAZO RAIA WAKE WANAFURAHA - GMK NEWS

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, March 18

RIPORT YA UMOJA WA MATAIFA JUU YA NCHI AMBAZO RAIA WAKE WANAFURAHA

Ripoti ya furaha ya Umoja wa Mataifa kwma mwaka huu inaonesha kuwa Finnland ndiko wanaishi watu wenye furaha au walioridhika zaidi duniani, ikifuatiwa na Norway, Denmark, Iceland na Uswisi. Kulingana na ripoti hiyo Burundi ndiyo inashika mkia katika orodha yenye jumla ya mataifa 156. Ripoti hiyo inaonesha kuwa Ujerumani inashika nafasi ya 15, Marekani nafasi ya 18 na Uingereza nafasi ya 19. China, licha ya kuwa ukuaji mkubwa wa kiuchumi, watu wake siyo wenye furaha sana ikiwa katika nafasi ya 86 kutoka 79 mwaka uliopita. Tanzania haiko mbali na Burundi ikishika nafasi ya 153, Rwanda katika nafasi ya 151 na Sudan Kusini iko katika nafasi ya 154. Ripoti hiyo inasema hata wahamiaji walioko kwenye mataifa yanayoshika nafasi za mwanzo pia ni wenye furaha kutokana na ubora wa maisha katika mataifa hayo. Ripoti ya furaha inazingatia vigezo sita: Kipato, matarajio ya kuishi, msaada wa kijamii, uhuru, imani na ukarimu.

No comments:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages