PATA SIMULIZI NZURI YA UPENDO - GMK NEWS

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, March 11

PATA SIMULIZI NZURI YA UPENDO

SIMULIZI:UPENDO.
SEHEMU 01.
..Simulizi Hii Mpya Iliyoanza Leo Inaitwa Upendo.Ni Simulizi Nzuri Inayogusa Na Yenye Kusisimua Tafadhali Usikose Hata Kipande Kimoja.Upendo Ni Hali Ya Kuwa Na Hisia Kwa Kile Ukipendacho,Kuchukuliana Mizigo Na Kuvumiliana.Lameck Ni Mtoto Aliyezaliwa Katika Jiji La Dar Es Salaam,Wilaya Ya Ilala Jimbo La Ukonga.Lameck Ni Mtoto Aliyezaliwa Katika Familia Ya Kimasikini Sana.Jina Lake Kamili Aliitwa Lameck Steven Peter.Lameck Alipokuwa Na Umri Wa Miaka Minne Aliweza Kuondokewa Na Baba Yake Kipenzi Aliyeitwa Steven Peter.Kabla Ya Baba Yake Na Lameck Kufariki Aliacha Watoto Wawili Lameck Pamoja Na Elisha.Elisha Alikuwa Akiishii Na Baba Yake Mkoani Mara Na Kule Alikuwa Akiishii Na Baba Yake Tu Na Hakuwa Na Ndugu Wengine.Elisha Kwa Muda Huo Kipindi Baba Yake Anafariki Yeye Alikuwa Anaumri Wa Miaka Ipatayo Nane.Ilichukuwa Muda Sana Mpaka Kuja Kujuwa Kuwa Mume Wake Alifariki Kwani Hapakukuwa Na Mtu Wa Karibu Ambaye Angeweza Kumpatia Taarifa.Mama Baada Ya Kupata Taarifa Hiyo Alisafiri Mkoani Mara Pamoja Na Mwanae Wa Mwisho lameck Aliyekuwa Anaishi Nae Mpaka Mahali Alipokuwa Mume Wake.Alipofika Alishangaa Kukuta Mazingira Yatofauti Kabisa Hakuweza Kugundua Mwanae Alipo Wala Hakuweza Kupewa Taarifa Yeyote Kuhusiana Na Mwanae Mkubwa Elisha Wala Mahali Alipozikwa Mume Wake.Hali Ile Ilimuuma Sana Mama.Mama Alikwenda Katika Kituo Kikubwa Cha Polisi Kutoa Taarifa Na Monchwari Pamoja Na Mahali Pa Watoto Yatima Lakini Kote Alizunguka Na Jitihada Zote Ziligonga Mwamba.Kwa Kweli Mama Yangu Alikuwa Akinipenda Sana Na Alikuwa Akimpenda Sana Baba Kwahiyo Tendo Lile Lilimchanganya Mamaa.Mara Baba Alikuwa Amekaa Kwenye Nyumba Ya Kampuni Kwahiyo Haikuwa Na Budi Kurejea Nyumbani.Tulirudi Na Kuja Kuendelea Na Maisha Yetu Ya Kimasikini Kama Kawaida.Mama Yangu Alikuwa Anajihusisha Na Uuzaji Wa Vitumbua Na Muda Mwingine Alikuwa Akiuza Miogo.Kwa Kweli Kwa Upande Wangu Mimi Sikuwa Na Kumbukumbu Nzuri Kwa Baba Yangu Kwani Siku Kaaga Nae Sana Alikuwa Ni Mtu Wa Kusafiri Mikoani Mikoani Kikazi Na Pia Nilikuwa Ni Mdogo.Lakini Pia Mungu Alitubariki Tulikuwa Tumeweza Kununuaga Kipande Cha Eneo Kidogo Kilichokuwa Bondeni Na Tulikuwa Tumejenga Vyumba Viwili Huku Chumba Hicho Kimoja Kikiwa Kinaningoja Mimi Nikue Kidogo Nikitumie Mana kwa Muda Huo Nilikuwa Ni Mdogo Nilikuwa Nina Lala Na Mama Nisingeweza Kulala peke Yangu Kwa Umri Wa Miaka Minne(4).Lakini Kubwa Jingine Zaidi Inasemekana Kuwa Tajiri Wa Baba Yangu Aliyekuwa Ikisemekana Kuwa Hana Uwezo Wa Kupata Mtoto Alimchukuwa Kaka Yangu Huyo Aliyekuwa Anaitwa Elisha Na Kumbadilisha Jina Na Kumwita Albert Na Kuishi Nae Kama Mwanae Wa Kumzaa Huku Elisha Au Albert Akiwa Hamkumbuki Na Kutokumjuwa Mama Yake Kwani Aliachana Na Mama Yetu Akiwa Na Umri Wa Miaka Mitano(5).Siku Zilizidi Kusogea Na Kufikia Mwaka Flani Mama Aliweza Kutunza Fedha Zake Na Kucheza Michezo Kama Mjuwavyo Wakina Mama Na Nilipofikisha Umri Wa Miaka Saba(7) Nilipata Kuanza Darasa La Kwanza Katika Shule Ya Msingi Na Pia Nilianza Sasa Kukaa Na Kulala Kwenye Kile Chumba Changu Kimoja.Miaka Ilianza Kwenda Nikiwa Shule Ya Msingi,Mama Alikuwa Akinisihi Sana Nisome Ilinije Kumsaidia Kwani Mama Alikuwa Yupo Radhi Hata Akope Ila Tu Mimi Niende Shule.Mama Aliweza Kunilipia Tution(Masomo Ya Ziada)Ili Kuhakikisha Ya Kwamba Nasoma Na Ninafaulu Kama Mjuwavyo Tution Inavyoaminiwa Ndio Jibu La Kufaulu Lakini Kwa Upande Wa Kaka Yangu Niliyekuwa Sijuani Nae Elisha Aliyebadilishwa Jina Na Kuitwa Albert Alikuwa Akisomeshwa Katika Shule Za Gharama Shule Za Kulipia Na Alikuwa Akiishi Maisha Ya Kitajiri Sana Kwa Upande Wa Albert Kwake Njaa Alikuwa Akiisikia Kwa Watu Lakini Kwa Upande Wangu Mimi Njaa Ilikuwa Ni Yangu Na Mama Yangu .Kwa Kweli Nilisoma Kwa Bidii Na Kwa Uchungu Sana Na Nilikuwa Napata Uchungu Pale Nilipokuwa Nikiona Mama Akikopa Baadhi Ya Vitu Kwa Ajili Yangu Nakushindwa Kulipa Na Kujikuta Akijificha Ili Asipate Kuonekana Na Mara Hata Kwa Mara Alikuwa Akisemwa Kwa Wale Waliyokuwa Wakimdai Mambo Yale Yaliniuma Sana Tena Sio Kidogo Yalinipa Muda Ya Kusoma Kwa Bidii.Nilizidi Kusoma Na Kusoma Huku Moshi Wa Kibatari Ukiishia Kwangu.Shuleni Walikuwa Wanitaniaga Bwana Mafuta Kwani Nilikuwa Nimtu Wa Kusumbuliwa Na Mafua Kila Mara Ni Kwasababu Ya Kibatari Ninachokuwa Nakitumia Nyumbani.Kwa Taswira Niliyokuwa Nayo Baada Ya Kukua Na Kutoka Kwenye Utoto Nilikuwa Ni Kijana Mrefu Wa Kimo Na Kijana Mweupe Kwa Kweli Kwa Upande Wangu Siku Muongeaji Sana Nilikuwa Na Hulka Ya Ukimya Hata Kama Nitakuwa Na Tatizo Linanisumbuwa.Waalimu Waliweza Kutambuwa Hulka Yangu Hiyo Na Hata Baadhi Yao Pale Nilipokuwa Ninamatatizo Waliweza Kugundua Na Kunisaidia,Kwa Kweli Nilikuwa Na Ukaribu Sana Na Waalimu Labda Nikutokana Na Kufaulu Kwangu Darasani.Nilipofika Darasa La Saba Mabadiliko Ya Kimwili Yaliweza Kuonekana Dhahiri Zaidi Ya Tulivyokuwa Darasa La Sita.Wanaume Kwa Wanawake Walikuwa Wamejiingiza Kwenye Mahusiano.
ITAENDELEA KESHO.
FUPI TAMU NDEFU INAKELA.USISAHAU KUTEMBELEA BLOG HII KWA MWENDELEZO WA HADITHI HII

No comments:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages